Watu wa jamii ya wasomali nchini
Afrika Kusini, wameandamana hadi bunge la la kitaifa mjini Cape Town
kupinga mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni nchini humo.
Waandishi wa habari wanasema kuwa mashambulizi dhidi ya waafrika wasio raia wa Afrika Kusini yameanza kutekelezwa katika siku za hivi karibuni.
Baadhi ya waandamanaji waliwashtumu maafisa wa utawala kwa kutochukua hatua zaidi kuwalinda raia wa kigeni , hususan wasomali.
Kulingana na kitengo cha haki za bindamu katika chuo kikuu mjini Pretoria,raia wa Afrika Kusini hawajakuwa wakionywa dhidi ya kuwashambulia raia wa kigeni .
Mwandishi wa BBC Mohammed Allie mjini Cape Town wanasema kuwa ghasia hizo zinahusishwa na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira, nchini Afrika Kusini.
Katika miaka ishirini iliyopita, maelfu ya wasomali wametoroka vita nchini Somalia na kuhamia Afrika Kusini ambako wameweza kuanzisha biashara ndogondogo katika sehemu za mijini.
No comments:
Post a Comment