Saturday, June 8, 2013

Mazungumzo ya amani yaendelea Mali

 

Mazungumzo yakiendelea mjini Ouagadougou, Burkina Faso.

Mazungumzo ya amani baina ya serikali ya Mali na wapinagaji wa Tuareg wanaomiliki eneo la Kidali Kaskazini mwa Mali yameanza nchini humo.

Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore ambaye anasimamia mazungumzo hayo kwenye mji mkuu wa Burkinabe,Ouagadougou ametaka kumalizika kwa mapigano mara moja ili kutoa nafasi ya kufanyika uchaguzi wa rais mwezi ujao.
Kumekuwa na rasha rasha za mapigano kwa siku za karibuni baina ya jeshi la Mali na vikosi vya wapiganaji wa Tuareg kwenye mji wa Kidali ambapo wanajeshi wa Mali wamezidi kusonga mbele kwenye mji huo ambao ndo mji pekee ambao bado upo chini ya waasi.

Tuareg na wapiganaji wa Kiislamu walishika miji kadhaa kwenye eneo la kaskazini mwa Mali lakini waliondolewa na majeshi ya Ufaransa ambayo yaliingilia kati mapema mwaka huu.

No comments:

Post a Comment