Thursday, June 6, 2013

Wanajeshi wa serikali wauawa Tunisia

 

Wanajeshi wa Tunisia wamekuwa wakikabiliana na wanamgambo mpakani mwa nchi hiyo.
Wanajeshi wawili wa Tunisia wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa katika shambulizi la bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara karibu na mpaka na Algeria.
Kwa mujibu wa duru za kijeshi, shambulizi hilo ni la hivi karibuni kufanywa dhidi ya wanajeshi wanaowasaka wanamgambo mpakani.
''Wanajeshi wawili wameuawa katika harakati zetu za kuwasaka wanamgambo,'' alisema msemaji wa jeshi Mokhtar Ben Nasr.
Mataifa ya Afrika Kaskazini, yamekuwa yakikabiliana na tatizo la wanamgambo tangu serikali kadhaa kung'olewa mamlakani ikiwemo, ile ya Libya, Misri na kadhalika.
Wapiganaji hao, wengi wao wenye uhusiano na kundi la al-Qaeda huvuka mipaka kwa urahisi katika kanda hiyo.
Mwezi Januari , wafanyakazi 48, waliuawa kufuatia vurugu katika kiwanda cha mafuta nchini Algeria.

Msako huo ulikuja baada ya majeshi ya Ufaransa kungia Mali kukabiliana na wapiganaji wa kiisilamu wanaoiahangaisha serikali ya nchi hiyo inayopakana na Algeria.
Tangu mwishoni mwa mwezi wa Aprili, takriban wanajeshi 20 nchini Tunisia wamejeruhiwa vibaya kwenye mashambulizi ya mabomu ya kutega ardhini yanayosemekana kutegwa na wapiganaji hao wa kiisilamu.

Katika shambulizi la hivi karibuni, bomu lilipuka wakati gari la jeshi lilipokuwa likisafiri katika eneo la Doghra karibu na mlima Chaambi, alisema bwana Ben Nasr.
Duru za kijeshi zinasema kuwa mmoja wa mwanajeshi aliyejeruhiwa huenda akakatwa mguu wake.
Serikali ya Tunisia imekuwa ikiongozwa kwa misingi ya dini ya kiisilamu, tangu kung'olewa mamlakani kwa rais Zine al-Abidine Ben Ali mwezi Januari mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment