Thursday, June 6, 2013

Vijusi wanaweza kuonyesha hisia tumboni

 

Vijusi wakijifunza kuonyesha hisia za uchungu wakiwa bado tumboni.
Vijusi au mtoto ambaye angali kuzaliwa akiwa bado kwenye mfuko wa uzazi, hujifunza kuonyesha hisia za uchungu wakiwa bado tumboni. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika vyo vikuu vya Durham na Lancaster nchini Uingereza.
Wanaamini kuwa vijusi hujifunza namna ya kuwasiliana baada ya kuzaliwa kwa njia za kulia au kwa kukunja uso wakiwa tumboni.
Utafiti huo uliofanywa kwa kupiga picha za Ultrasound, ulionyesha kuwa vijusi hujifunza kusonga na kuonyesha hisia wakati wakiwa tumboni.
Picha hizo zilionyesha hisia za vijusi hao wakati wa ujauzito wakionekana wakicheka, au kutabasamu, kukunja uso na hata kuvuta pua.

Mtafiti mkuu Daktatri Nadja Reissland, alisema kuelewa namna ambavyo mtoto anakuwa tumboni, inaweza kuwasaidia madaktari kujua ikiwa kuna matatizo yoyote na watoto kabla ya kuzaliwa.
"haijulikani ikiwa vijusi wanaweza kuhisi uchungu au haijulikani ikiwa kwa kukunja uso ni ishara tosha kuonyesha ikiwa vijusi wanahisi uchungu,'' alisema daktari huyo.
Utafiti ulionyesha kuwa mkunjo wa uso ni dalili ya ubongo kukuwa kuliko kuonyesha hisia za uchungu.
Utafiti ulitumia kanda ya video iliyokuwa na picha tatu za Ultrasound za vijusi wanane wasichana na saba wavulana.

Utafiti huu unakuja baada ya utafiti uliofanywa hapo awali ukipendekeza kuwa vijusi wenye afya nzuri huendelea kukuwa wakati ujauzito ukiendelea kukoma.
Daktari Reissland, mtafiti mkuu katika chuo kikuu cha Durham, amesema kuwa ni muhimu kwa vijusi kuonyesha hisia za uchungu mara wanapozaliwa ili waweze kuonyesha ikiwa wana uchungu huku wakirahisisha mawasiliano na wazazi wao.

No comments:

Post a Comment