Mahakama ya rufaa nchini
Uingereza imebatilisha uamuzi uliotolewa na mahakama kuu mjini London,
uamuzi ambao huenda ukawa na athari kubwa kwa wanandoa wanaokwenda
mahakamani kutalikiana.
Mahakama hiyo ya rufaa iliagiza kuwa mali na
hisa ya mfanya biashara mmoja raia wa Uingereza mwenye asili ya Nigeria,
katika kampuni mbali mbali zijumuishwe katika orodha mali
watakayogawana.Majaji katika mahakama hiyo ya rufaa waliagiza kuwa mali yote inayomilikiwa na mfanyabiashara huyo binafsi na katika makumpuni tofauti katika sehemu mbali mbali duniani ni lazima yajumuishwe.
Mkewe, tajiri huyo, Yasmin Prest amesema amefurahishwa sana na uamuzi huo wa mahakama.
Lakini Bwana Prest alifahamishwa mahakama kuwa, hamiliki pekee mali yake inayokisiwa kuwa mamilioni ya madola.
Hata hivyo majaji hao walisema kuwa uamuzi wa mahakama kuu uliotolewa Oktoba mwaka uliopita, wa kumlazimisha bwana Prest kuhamishwa mali yake kutoka kwa kampuni anazomiliki kwa pamoja na watu wengine, sio halali.
Lakini Bi. Prest alikwasilisha rufaa katika mahakama ya juu zaidi kutoka kesi hiyo kusikilizwa upya.
Katika uamuzi wake mahakama hiyo ya rufaa ilisema kuwa kampuni hizo tofauti zinamiliki mali hiyo kwa niaba ya bwana Prest.
Kesi hiyo sasa itaangaziwa pakubwa na familia tajiri, hasa wale kutoka nje ya Uingereza.
Kwa mujibu wa wakili mmoja William Longrigg, mahakama imeonekana kuanza kuwalinda wanyonge na wale wasiokuwa na mali katika ndoa.
Vile vile amesema uamuzi huo wa kubainisha kuwa mali inayomilikiwa na kampuni ni mali ya mtu binafsi ni mwanzo wa kutambua mali hasa kwa wale wanaoficha mali yao katika makampuni wakati wanapotengana na wakeo.
Mahakma hiyo ilifahamishwa kuwa Prest ana mali inayokisiwa kuwa pauni milioni 48, lakini mkeo alikanusha madai hayo na kusema kuwa huenda ni inazidi pauni milioni mia moja.
Wawili hao walifunga ndoa mwaka wa 1993 na tangu wakati huo wamekuwa wakiishi mjini London.
Wakati wa kesi, Bwana Prest alituhumiwa kwa kukosa kusema ukweli kuhusu mali yote anayomiliki.
Jaji Lord Sumption alisema kuwa ushahidi wake ulijawa na udanganyifu mkubwa na alijaribu kuficha ukweli wa mambo.
No comments:
Post a Comment