Takriban watu 180 wamekamatwa
nchini Afrika Kusini wakibeba karatasi za plastiki zenye kinyesi cha
binadamu , kabla ya maandamano makubwa kufanyika wakilalamikia serikali
kukosa kudumisha usafi mjini Cape Town.
Licha ya watu kukamatwa, katarasi kadhaa zilizokuwa na uchafu huo , zilitupwa ndani ya ofisi za wizara ya serikali za mitaa .Ni waziri wa mkoa wa Western Cape, ambao ndio mkoa pekee usiokuwa chini ya uongozi wa chama cha ANC.
Mwandishi wa BBC mjini Cape Town, Mohammed Allie, anasema kuwa hapana shaka kuwa matizo ya ukosefu wa usafi ni kero kubwa mjini Cape Town, lakini watu wengi wanahoji kwa nini maandamano haya yamefanyika mjini humo pekee wakati tatizo hilo ni kero pia katika miji mingine.
Chama cha ANC, kimejitenga na ambavyo maandamano hayo yanafanywa.
Wakati huu , wenyeji wa mitaa mingi hutumia vyoo kwa pamoja , ambavyo usafi wake ni duni sana na hata wanawake wamekuwa wakibakwa katika sehemu hizo nyakati za usiku.
Waandamanaji walikuja kwa treni kutoka mitaa inayopakana na Cape Town wakiwa na karatasi zenye kinyesi kabla ya kuzuiliwa na polisi.
Mwakilishi mmoja wa mtaa, aliyefukuzwa kutoka chama cha ANC, ni miongoni mwa waliokamatwa.
"tunaondoa kinyesi kwenye vyoo vyetu, kwa sababu vyoo hivyo, vimekuwa vikinuka kwa miezi mitatu sasa,'' aliambia jarida la Eyewitness News.
Waandamanaji, wanatuhumu wizara ya kushughulikia maslahi ya mitaa inayoongozwa na chama cha Bi Zille Democratic Alliance, kwa kutofanya kazi 'inavyotakikana, ikiwemo kuboresha mazingira kwa wakaazi wa mitaa.
Hata hivyo chama cha DA kinasema kuwa hakina uwezo wa kufanya yote wanayoyataka wakaazi wa eneo hilo.
Imekuwa ikiwapa wakaazi vyoo vya kuhamishwa hamishwa lakini wakaazi wanasema hilo halitoshi.
Waandamanaji waliamua kutumia kinyesi kutoka kwa vyoo hivyo katika maandamano yao , ambayo vyombo vya habari nchini humo vimeitaja kuwa vita vya kinyesi.
Wiki jana waandamanaji walitupa kinyesi hicho nje ya majengo ya bunge.
No comments:
Post a Comment