Monday, June 10, 2013

Mkuu wa majeshi ya Libya ajiuzulu

     

Waandamanaji wanaounga mkono serikali wakiandamana dhidi ya wanamgambo wenye silaha huko Tripoli, Libya, May 3, 2013.
Waandamanaji wanaounga mkono serikali wakiandamana dhidi ya
wanamgambo wenye silaha huko Tripoli, Libya, May 3, 2013.
                       
Mkuu wa jeshi la Libya amejiuzulu baada ya mapigano kati ya waandamanaji na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali kupelekea kufariki kwa  watu 31 katika mji wa mashariki wa Benghazi.

Ghasia zilizuka  Jumamosi wakati waandamanaji mjini  Benghazi walipovamia ngome ya kundi la wanamgambo wa kiislam  wanaolipwa na serikali  kusaidia kulinda usalama.

Waandamanaji hao walikuwa wanadai wanamgambo waweke silaha chini na kujisalimisha kwa maafisa wa majeshi ya Libya.
Mkuu wa majeshi ya Libya Youssef al Mangush ambaye alikuwa msimamizi wa wanamgambo alijiuzulu  Jumapili. Mkuu huyo amekosolewa kwa kuchelewa kuunda jeshi la kitaifa na kuwaacha wanamgambo waongezeke.

No comments:

Post a Comment