Monday, June 10, 2013

Kundi la LRA lajihusisha na biashara ya meno ya tembo

  

Caesar Achellam, kamanda wa cheo cha juu wa kundi la LRA
Caesar Achellam, kamanda wa cheo cha juu wa kundi la LRA.
                      
Ripoti mpya imesema kwamba kuna ushahidi  mkubwa kuwa kundi la waasi la (LRA) linajishughulisha na ujangili wa  meno ya  tembo huko Afrika ya kati.

Taarifa hiyo iliyotolewa Jumatatu , inasema  LRA wanatumia biashara hiyo haramu ya meno ya tembo kama njia ya kujikimu.

Ugunduzi unatoka katika  mashirika mawili yenye makazi yake   Marekani, mradi wa Enough,  na mradi wa  satellite Sentinel kulingana na uchunguzi  uliofanyika katika hifadhi ya  taifa ya wanyama ya Garamba katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Msemaji wa mradi  wa Enough Jonathan Hutson hivi karibuni alitembelea hifadhi  hiyo. Katika mahojiano na VOA amesema   mfungwa wa zamani wa LRA ni mmoja wa wale walioelezea ukatili katika eneo hilo.

Hutson anasema mfungwa huyo anasema  ameona wapiganaji wa LRA wakipiga risasi tembo na kukata nyama za maiti ya tembo hao.
Na wanachama wengine wa LRA waliojitoa  katika kundi hilo wanaripoti kwa nyakati tofauti waliona helikopta nyeupe zikituwa kwenye mbuga hiyo na kununua pembe za ndovu kwa kuwapa wapiganaji silaha,bunduki na vyakula.

LRA wakati fulani walipambana na serikali ya  Uganda lakini kwa sasa wamekuwa ni kikosi cha wapiganaji wanaozunguka zunguka  huko Congo, Sudan Kusini na Jamhuri ya  Afrika ya kati.

No comments:

Post a Comment