Wananchi wa mtwara hawataki gesi asilia kusafirishwa popote.
Mbunge wa jimbo la Mtwara, eneo
ambalo limekumbwa na vurugu hivi karibuni kusini mwa Tanzania
amefikishwa mahakamani leo akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi wa vurugu
zilizo sababisha vifo vya watu watatu mwezi uliopita.
Hasnain Murji pamoja na watuhumiwa wengine 91 wamefikishwa kwenye mahakama ya wilaya ya Mtwara.
Kwa muda huu baadhi ya watuhumiwa
wamepata dhamana huku wengine wakiendelea na taratibu za kukamilisha
udhamini, wakati Mbunge huyo akisubiri kupandishwa kizimbani na kusomewa
mashtaka yanayo mkabili.
Wananchi waliofika mahakamani kwa ajili ya
kusikiliza kesi zinazowakabili ndugu na jamaa zao wamelalamikia
utaratibu wa kuwazuwia kuingia mahakamani hapo.
Mbunge huyo wa Chama kinacho tawala nchini humo CCM, alikamatwa na kushikiliwa na jeshi la Polisi mkoani humo siku ya Jumamosi.
Idadi kubwa ya wananchi wa Mtwara wamekuwa
katika mvutano mkali na Serikali ya Tanzania ambayo imekusudia kujenga
bomba la kusafirisha gesi asilia inayopatikana mkoani humo hadi Dar es
Salaam , Hatua inayopingwa na wananchi hao ambao wanadai gesi hiyo
isisafirishwe na kupelekwa popote.
No comments:
Post a Comment