Monday, June 10, 2013

Mazungumzo ya Kampala juu ya DRC huwenda yakaanza wiki hii

 


wapiganaji wa M23 wakiondoka kutoka Masisi na Sake mashariki ya Kongo, Nov 30, 2012.
Wapiganaji wa M23 wakiondoka kutoka Masisi na Sake mashariki ya
Kongo, Nov 30, 2012.
                       
Viongozi wa wapiganaji wa kundi la waasi la M23 kutoka mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanaeleza matumaini kwamba duru mpya ya mazungumzo ya Kampala yanayotarajiwa kuanza baadae wiki hii yataweza kuleta ufunmbuzi kwa matatizo ya usalama mashariki ya nchi yao na kupelekea amani ya kudumu.


Akizungumza na Sauti ya Amerika kutoka Kampala mpatanishi mkuu wa M23 Kambasu Ngeve anasema matumaini yao ya ufanisi unatokana na kwamba jumuia ya kimataifa imefahamu vyema matatizo yao nawamepata motisha ya kujadili kwa dhati.
Mwakilishi maalum kwa ajili ya mataifa ya kanda ya Maziwa Makuu, Bi. Mary Robinson alipongeza tangazo la uwezekano wa kuanza mazungumzo ya Kampala kati ya sderikali ya Kinshasa na waasi wa M23.

Anasema wamerudi Kampala kufuatia wito wa wakuu wa Umoja wa Mataifa hasaa baada ya ziara ya Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika kanda ya maziwa makuu mwezi uliyopita.

Bw. Ngeve anasema wakati wa duru hii ya majadiliano, hawatoendelea tena na madai ya awali ya kutaka kuundwa serikali ya mpito na mabadiliko ya katiba bali wanataka kuzungumzia masuala ya usalama na amani kwa watu wa mashariki ya DRC.

No comments:

Post a Comment