Maelfu ya waandamanaji
wameandamana katika barabara za mjini Addis Ababa, Ethiopia, wakidai
waandishi wa habari na wanaharakati walioko kizuizini wafunguliwe.
Makundi ya kutetea haki za kibinaadamu yanasema serikali imetumia sheria za kupambana na ugaidi ili kuwafunga waandishi wa habari.
Waandamanaji- wengi kutoka upinzani - walipiga kelele kudai uhuru na haki.
Haya ni maandamano ya kwanza tangu mwaka wa 2005 ambapo mamia ya waandamanaji waliuliwa katika ghasia zilizofuatia uchaguzi.
No comments:
Post a Comment