Wizara ya fedha ya Afrika Kusini
inachunguza tuhuma kwamba mali ya thamani ya kama dola bilioni moja ya
Libya ilifichwa nchini humo.
Jacob Zuma, kushoto, na aliyekuwa kiongozi wa Libya Marehemu Kanali Muamar Gaddafi, kulia.
Serikali ya Libya imekuwa ikijaribu kuzipata mali za Kanali Gaddafi katika sehemu mbali-mbali za dunia tangu alipofariki mwaka 2011.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema watu wengine wamekisia kuwa mali ya hayati Gaddafi ilioko nchi za nje inaweza kufika dola bilioni 80.
No comments:
Post a Comment