Japan imeahidi kutoa dola
bilioni 32 za msaada na uwekezaji katika Afrika, ikijaribu kulingana na
Uchina ambayo ina uhusiano mkubwa zaidi wa kiuchumi na bara hili.
Msaada utalenga miradi ya kujenga miundo mbinu na usafiri ndani ya miji pamoja na uzalishaji wa nishati.
Waziri Mkuu wa Japani, Shinzo Abe, aliwaambia wajumbe katika mkutano wa maendeleo ya Afrika unaofanywa mjini Yokohama, kwamba umuhimu utapewa uwekezaji wa kibinafsi.
Alisema: "Mali asili nyingi ya Afrika inatoa fursa muhimu ya biashara na Japan ambayo haina mali asili.
Lakini Japan haitotafuta na kuchimba mali asili kuzileta Japan tu.
Tutaisaidia Afrika ili mali asili ya Afrika ikuze uchumi wa Afrika.
Na soko la Afrika linalokua haraka pia ni muhimu kwa makampuni ya Japan"
No comments:
Post a Comment