Shirika la ndege, linalotoa
huduma za usafiri wa ndege kwa bei nafuu Fastjet, limepata kibali cha
kuanzisha safari za ndege za kimataifa za bei nafuu, kutoka Tanzania
hadi Afrika Kusini, Zambia na Rwanda.
Kampuni hiyo inayomilikiwa na Stelios
Haji-Ioannou, ambaye ni mmiliki wa shirika la ndege la Easyjet, lililo
na makao yake barani ulaya.Kwa sasa shirika hilo linahudumia wasafiri nchini Tanzania pekee.
Raia wengi na hasa wafanya biashara wamefurahishwa na tangazo hilo, wakisema kuwa itapunguza gharama za usafiri na hivyo kuimarisha biashara katika kanda hiyo.
Nchini Kenya, shirika la ndege la Kenya Airways ambalo ni moja ya mashirika makubwa ya ndege barani Afrika, limepata pigo kubwa baada ya kupata hasara kubwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Ripoti zinasema kuwa shirika hilo lilipata hasara ya zaidi ya dola milioni mia moja kabla ya kutozwa ushuru, kiwango ambacho ndicho mbaya zaidi tangu mwaka wa 2009.
Shirika hilo lilikuwa maarufu sana kwa abiria wanaosafiri magharibi, mashariki, kusini na katika mataifa ya Afrika ya kati.
No comments:
Post a Comment