Sehemu yenye utata ya Abyei inasimamiwa na mamlaka maalum ya muda.
Kiongozi maarufu wa kimila katika eneo la Abyei ameuawa kwa kupigwa risasi katika tukio lililohusisha wapiganaji wa kiarabu.
Kiongozi huyo Kual Deng Majok ambaye ni kiongozi
mkuu wa ukoo wa Dinka aliuawa katika mapambano kati ya Kundi la
Wapiganaji wa kiarabu la Misseriya na walinzi wa amani wa Umoja wa
mataifa ambapo imeelezwa kuwa maafisa wa Kijeshi wa Umoja wa mataifa pia
walijeruhiwa katika tukio hilo.
Jimbo
la Abyei lenye utajiri wa mafuta linalogawanya lililo kati kati ya
Sudan na Sudan kusini lilijitenga mwaka 2011,ambapo umiliki wake
unagombewa na nchi zote mbili.
Chanzo cha mgogoro huo ni ugomvi wa ardhi kati
ya Wakulima wanaoungwa mkono na serikali ya Sudan kusini wa kabila la
Dinka Ngok na wafugaji wa Misserya wanaotoke upande wa kaskazini.
Kutokana na mgogoro Jimbo la Abyei limeendelea kuwa chiniya usimamizi wa Umoja wa vikosi vya umoja wa mataifa.
Sehemu ya Abyei.
Tukio hilo la Jumamosi lilianza wakati vikosi
vya jeshi la umoja wa mataifa lilipojaribu kuwaokoa maofisa wa kijeshi
wa Sudan kusini wanaofuatilia hali ya baadae ya Jimbo la Abyei,baada ya
kuzingirwa na wapiganaji wa Misseriya.
Msemaji wa Kundi la Dinka aliwaambia waandishi
wa habari kuwa Kiongozi wao mkuu Kual Deng Majok aliuawa baada ya
kushambuliwa na wapiganaji wa Kundi la Misseriya,ambapo tukio hilo pia
limethibitishwa na mkuu wa kundi la Misseriya,ambaye kwa upande wake
amesema wapoganaji wa Kundi la Misseriya walisimamisha msafara wa
maafisa wa sudan kusini na kuanza majadiliano ambapo askari mmoja katika
jeshi la Umoja wa mataifa alimpiga risasi mpiganaji mmoja wa kundi hili
aliyekuwa akijiandaa kutoa silaha yake.
Sudan na Sudan kusini zimekuwa katika kipindi
kirefu migogoro ya kidini na kikabila kilichosababisha vita ya kikabila
ambavyo vimegharimu maisha ya watu zaidi milioni moja na nusu
abyei_arab_wapiganaji
No comments:
Post a Comment