Sunday, May 19, 2013

Polisi wa Nairobi wauwa washukiwa wawili

Polisi mjini Nairobi, Kenya, wamewapiga risasi na kuwauwa watu wawili - mwanamume na mwanamke - baada ya watu hao kurusha maguruneti mane na kuwajeruhi askari kama watano.
                    
Polisi wa Nairobi wakiwa kazini

Polisi walivamia ghorofa wanakoishi watu hao kwenye kitongoji cha mji na waliwaamrisha watoke nje ya ghorofa.
Wakuu wa polisi wanasema wawili hao walikataa kusallim amri, walirusha maguruneti na walimtumia mtoto wao mchanga wa miezi minane kuwa kinga.
Haijulikani kama watu hao wawili wanahusika na kundi lolote la wapiganaji.
Magazeti ya Kenya yanaarifu kuwa kisa hicho kilitokea katika Githurai estate.

No comments:

Post a Comment