Sunday, May 5, 2013

Mahakama ya Kenya yawakuta na hatia Wairan wawili

 

Wairan wawili wakiwa mahakamani Kenya, Sayed Mansour Mousavi (kushoto) and Ahmed Abolfathi Mohammed, kuliaWairan wawili wakiwa mahakamani Kenya, Sayed Mansour Mousavi (kushoto) and Ahmed Abolfathi Mohammed, kulia.

               
Mahakama moja nchini Kenya imewakuta na hatia raia wawili wa Iran kwa kupanga kushambulia kiwa bomu vituo vya nchi za magharibi na Israel nchini Kenya.

Jaji  Kaire Waweru alisema alhamis upande wa  mashtaka umethibitisha bila ya mashaka tuhuma zote dhidi ya washtakiwa  hao wawili.

Ahmad Abolfathi Mohammad na Sayed Mansour Mousavi walishtakiwa kwa kujiandaa kufanya uhalifu wenye nia ya uharibifu mkubwa  baada ya kukamatwa Juni mwaka 2012 na kukutwa na maafisa wa usalama wakiwa na kilo 15 za milipuko aina ya RDX.

Mawakala hao wa  Iran wanashutumiwa katika mashambulizi au kuandaa mashambulizi ulimwenguni kote katika miaka ya karibuni ikiwemo  nchini Azerbaijan, Thailand na India. Njama nyingi ambazo zilibainisha  kuilenga Israel.

Maafisa wa kupambana na ugaidi nchini Kenya walisema wa-Iran hao  ni wanachama wa kitengo cha  Islamic Revolutionary Fuards Corps Quds Force nchini Iran.



No comments:

Post a Comment