Kazi za uokozi zilizokuwa
zikifanywa Darfur, Sudan, kutafuta wafanyakazi 100 walionasa kwenye
mgodi wa dhahabu ulioporomoka Jumatatu zimesimamishwa.
Hakuna aliyenusurika.
Inaarifiwa kuwa migodi midogo-midogo ya Sudan ilitoa dhahabu ya thamani ya zaidi ya dola bilioni-mbili mwaka jana.
Madini hayo yanaipatia Sudan sarafu za kigeni ambazo zilipungua sana baada ya Sudan Kusini kujitenga mwaka wa 2011 na kubaki na visima vingi vya mafuta.
No comments:
Post a Comment