Msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulaigye.
Hata hivyo baadhi wanadai kuwa wanajeshi haswa wanaotoka katika maeneo ya hatari hawapewi huduma za kuwatuliza kisaikolojia jambo ambalo limekanushwa na jeshi.Mwandishi wetu wa Kampala Siraj kalyango na maelezo zaidi.
Mwanajeshi huyo, Private Patrick Okot,anakabiliwa na mashtaka kadha yakiwemo, mauaji, wizi wa kutumia nguvu pamoja na kushindwa kutumia vizuri mali ya jeshi.
Katika kikao cha leo, mahakama ya kijeshi imearifiwa kuwa mshatakiwa hana kasoro yoyote ya kiakili.
Shahidi namba 16 ambaye ni daktari wa upasuaji katika hospitali kuu ya Mulago aliyefanyia uchunguzi miili yote ya waathirika ,ameiambia mahakama kuwa miili yote 10 ilikuwa na majeraha ya risasi.
Baadhi ya makundi yasiyo ya kiserikali yanadai kuwa matukio mbalimbali ya wanajeshi hasa kupiga risasi raia,baada ya kurejea kutoka vitani, kunaashiria matatizo yaliyopo ndani ya jeshi ukiwemo ukosefu wa kuwapa huduma za kisaikolojia .
Wanajeshi wa Uganda walipopata ajali Kenya wakielekea Somalia.
Lakini msemaji wa masuala ya siasa jeshini Kanali Felix Kulaigye anapinga madai hayo.
Hii italazimu mahakama ya kijeshi kufanya vikao vyake kwa siku tatu mfululizo kila wiki kuanzia Jumatatu, Jumanne na Jumatano.
No comments:
Post a Comment