Wednesday, June 26, 2013

Wanajeshi wapya wa UN kushika doria Mali

Mali ingali inakabiliwa na changamoto si haba za kiusalama Baraza la usalama la Umoja wa mataifa, limekubali kuwa kikosi cha usalama chenye wanajeshi 12, 600 kipelekwe nchini Mali ifikapo tarehe moja mwezi Julai.
Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa, alisema kumekuwa na makubaliano ya pamoja, kuwa wanajeshi wa UN wapelekwe Mali kuchukua hatamu kutoka kwa wanajeshi wa Afrika wanaoshika doria huko.


Umoja wa mataifa utatii mpango uliowekwa mwezi Aprili.
Wanajeshi wa kimataifa, waliingilia kati mgogoro wa kisiasa nchini Mali, kukomeshwa harakati za wapiganaji wa kiisilamu mjini Bamako.
Kikosi kipya cha UN kijulikanacho kama 'Minusma', kitakabiliwa na changamoto za kisiasa na kiusalama na watafanya kazi katika mazingira ya joto kali.

Kikosi hicho, kitalenga kuweka mazingira ya usalama, kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao tarehe 28 mwezi Julai.
Kwa sasa bado kuna makabiliano kati ya makundi ya wapiganaji wa kiisilamu na waasi wa Tuarag, kulingana na balozi maalum wa Umoja wa mataifa nchini Mali Albert Koenders.
Aliongeza kuwa kutakuwa na changamoto kubwa kwa mchakato wa uchaguzi kulingana na mpangilio wa sasa.

Ufaransa, ambayo ndiyo nchi yenye wanajeshi wake wengi nchini Mali , imesema wanajeshi efu moja wataendelea kuhudumu katika kukabiliana na harakati dhidi ya ugaidi.
Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa, Mark Lyall, alisema kuwa kikosi kipya cha kulinda amani, kiotawahusisha wanajeshi wa kiafrika wlaioko mali tayari.
Sasa wana miezi minne kuhakikisha wametimiza viwango vinavyohitajika vya umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu pamoja na kuwa na vifaa vya kutosha.
Mkuu wa haki za bindamau katika UN Herve Ladsous,alisema kuwa nchi ya Chad itachunguzwa vilivyo hasa kutokana na rekodi yake ya kutumia watoto kama wanajeshi.

No comments:

Post a Comment