`Maafisa wa uhamiaji nchini Ghana wanasema kuwa polisi wamewakamata zaidi ya raia 150 wa uchina ambao wanashukiwa kuhusika na uchimbaji wa dhahabu kinyume na sheria.
Kulingana na Francis Palmdeti kutoka idara ya uhamiaji nchini Ghana,raia hao wanazuiliwa katika migodi minne tofauti nchini humo.Hata hivyo msemaji wa ubalozi wa uchina nchini Ghana anasema kwamba anataraji kuwa raia hao watarudishwa makwao.
Wakati huohuo, wizara ya mambo ya kigeni ya Uchina imelalamikia serikali ya Ghana baada ya wafanyakazi hao wa China kuzuiliwa kufuatia msako uliofanywa wa wachimbaji haramu wa madini.
Ghana ndiyo nchi yenye kuzalisha kiwango kikubwa cha Dhahabu baada ya Afrika Kusini barani Afrika.
Huku bei ya dhahabu ikiendelea kupanda katika miaka ya hivi karibuni, sekta hiyo imekuwa ikikumbwa na wachimbaji haramu wa madini hayo ikiwemo, idadi kubwa ya wafanyakazi wa kichina inayoendelea kuongezeka. China imesema kuwa intaka watu hao kutoteswa na kutoibiwa wakati wa msako huo.
No comments:
Post a Comment