Sunday, June 2, 2013

Vita vya Syria vyazidi kutapakaa Lebanon

Katika ishara nyengine kuonyesha jinsi vita vya Syria vinavoathiri taratibu utulivu katika nchi ya jirani ya Lebanon, askari huko wanasema wapiganaji kadha wa Syria waliuwawa Jumamosi usiku katika mapambano na vikundi vya Hezbollah nchini Lebanon karibu na mpaka wa Syria.   
                  
Wapiganaji wa Libnan wanaosaidia serikali ya Syria wakiwa zamu kwenye mpaka na Syria

Inaarifiwa mapigano hayo yalitokea mashariki mwa bonde la Bekaa katika mji wa Baalbek.
Jumamosi makombora na mizinga kadha ilirushwa dhidi ya eneo hilo na makombora zaidi yamepiga piya mitaa ya kusini mwa Beirut.
Wapiganaji wa Syria wamesema watafanya mashambulio ndani ya Lebanon kulipiza wapiganaji wa Hezbollah kumsaidia kivita rais wa Syria, Bashar al Assad.

No comments:

Post a Comment