Wednesday, June 12, 2013

Utulivu warejea mjini Istanbul, Uturuki

 

Maandamano mjini Istanbul.
 
Maafisa wa Uturuki wamedhibiti tena bustan ya Taksim mjini Istanbul, baada ya polisi wa kupambana na ghasia kutumia gesi ya kutoa machozi na magari ya kurusha maji kuwatimua waandamanaji wanaoipinga serikali.
Mwandishi wa BBC aliyepo katika eneo hilo anasema takataka bado zimetapakaa pamoja na magofu ya magari yaliyoteketezwa moto lakini hali imetulia kwa sasa.
Waandamanaji wengi wamekusanyika tena karibu na bustani ya Gezi ambayo ndiyo imekuwa chanzo cha ghasia hizo baada ya kusemekana kuwepo mpango wa kuukarabati.
Waziri mkuu amesema kuwa maafisa wa usalama hawatakubali au kustahamili watu wenye nia ya kuharibu Uturuki.
Waandamanaji hao wanamtuhumu waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan kwa kujipatia mamkala zaidi na kujaribu kuweka sheria kali za kiisilamu katika nchi isiyo fuata misingi ya dini.
Ilidhaniwa kuwa waziri mkuu angekutana na waandamanaji Jumatano, katika juhudi zake kutaka kufanya mazungumzo naye.

Lakini sasa ni bayana kuwa mazungumzo yatafanyika na wapatanishi akiwemo muigizaji mmoja mwanamke na mwandishi .
Vuguvugu la waandamanaji hata hivyo halijaalikwa kushiriki kwa mazungumzo hayo na kusema kuwa haiwatambui walioteuliwa.
Kwa hivyo huenda mazungumzo hayo yasiafikie chochote. Kwa sasa bustani ya Taksim, imetulia.

No comments:

Post a Comment