Tuesday, June 25, 2013

Upinzani dhidi ya chama cha ANC

 

Dokta Mamphela Ramphele.
Huku chama kipya cha kisiasa kikizinduliwa rasmi nchini Afrika Kusini, takriban miongo miwili tangu kumazilika kwa enzi ya ubaguzi wa rangi, je chama hiki kinaweza kufanikiwa katika azma ya kutwaa utawala wa nchi hiyo?
"Wanatuibia , sasa tunawezaje kuwapigia kura,? anahoji Kaiser Kangwana mwanachama wa chama tawala ANC, ambacho viongozi wake katika mkoa wa Eastern Cape wamekuwa wakihusishwa na kashfa za ufisadi.


Bwana Kangwana, aliyetoa kijasho amekuwa akijitafutia riziki katika machimbo ya madini kwa miaka mingi, sasa ni mmoja wa wapiga kura walioishiwa na matumaini na ambao chama hiki kipya, chake Dokta Mamphela Ramphele kinalenga kuvutia.
Kofia aliyovalia bwana Kangwana yenye nembo ye chama cha ANC, inaonyesha wazi kuwa amekasirishwa sana na chama tawala.
"Watu wengi hapa hawana kazi , wangali maskini , '' anasema Kangwana.

Chama hiki kipya, ambacho kinaongozwa na Dokta Ramphele kinaitwa, Agang. Kikimaanisha ''ujenzi'' kwa lugha ya Sepedi.

Lengo kuu la chama ni kuwaunganisha wananachi wa Afrika Kusini, na kuwahamasisha kuzingatia msingi wa demokrasia ambao rais wa zamani Nelson Mandela alikuza kufuatia vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Ni Sifa ya Mandela ambayo baadhi wanaamini kuwa inapondwa na chama cha ANC, chama ambacho daima kinashutumiwa kwa kukosa kutoa huduma muhimu kwa wananchi ikiwemo, kuhakikisha wana maji safi, nyumba na kazi.

Chama cha AGANG, kinachounga mkono maswala ya kibiashara na kupinga ufisadi, bado hakitajangaza sera zake lakini kinaonekana kutaka kuhakikisha kuwa wanasiasa wanawajibika, wafanyakazi wa umma kufanya kazi ipasavyo na kupatia Elimu kipaombele katika ajenda yake ya kisiasa.
Wafuasi wake, wanaamini kuwa mpango wa kuwawezesha kiuchumi waafrika weusi nchini humo, badala yake umewaimarisha wachache tu na wanaamini kuwa kima cha dola bilioni 2.9 pesa za umma ambazo hufujwa kila mwaka zinaweza kutumiwa vyema tu kwa mpango wa kuimarisha maisha ya watu nchini humo.
Hata hivyo kuna hofu kuwa chama cha Agang huenda kikawa tu chama cha mtu mmoja.

Dokta Ramphele ni mtu mwenye sifa nzuri , na ambaye wengi wanamfahamu kwa kupigania haki , baadhi ya mambo yanayowashawishi wapiga kura. Anafahamika kama daktari aliyefanya kazi yake katika mkoa wa Eastern Cape pamoja na mumewe aliyepigania uhuru wa Afrika kusini, Steve Biko, Dr Ramphele laliongoza harakati za mashinani dhidi ya utawala wa ubaguzi wa kibaguzi miaka ya sabini.
Miaka ishirini baadaye utawala huo ulisalimu amri na waafrika weusi wakaingia uongozini.
Daktari, Ramphele amewahi kuwa afisaa mkuu mtendaji wa benki ya dunia, naibu chansela wa chuo kikuu cha Cape Town,hadi hivi karibuni alikuwa mwanachama wa bodi la halmashauri ya kampuni moja ya madini.
Kumeshuhudiwa maandaano makubwa kupinga huduma duni kwa wananchi katika baadhi ya maeneo ya nchi.

 
 
Rampehele ansemekana kuwan nan sifa nzuri lakini chama chake sio tisho kwa ANC.
Lakini kikubwa kinachosalia ni kuwa ana sifa nzuri kikazi na hii huenda ikawa kikwazo kwa azma yake.
Wadadisi wa kisiasa wanasema kuwa kwa kuwa mama juyu ndiye mtu pekee mwenye sifa kumwezesha kuwa kiongozi katika chama chake,itakuwa changamoto kubwa. Tumeshuhudia mambo kama haya nama vyama kama hivi kawaida havifanyi vizuri kisiasa.
Chama kimeundwa na wananchi ambao hawajawahi kupiga kura au ambao hawajawahi kuwa wanachama wa vyama vya kisiasa.

Chama cha ANC hakimuoni Dokta Ramphele kama tishio kubwa.
Chama kipya cha kisiasa ambacho kinalenga kuzungumzia maswala ya ufisadi, hupata kupendwa na wengi, wakati wananachi kwa kweli hawana matumaini mengi na chama cha ANC kuhusiana na uwajibikaji wa wanasiasa wake.
Lakini kijana Sibusisu Segwane, ambaye amefuzu chuo kikuu, mjini Johannesburg, huenda bado akakipigia kura chama cha ANC.
Ingawa anavutiwa na Ramphele, anahofia kupoteza kura yake.

“ANC ni chama pekee chenye ujuzi wa kuendesha serikali,” anasema
Ni kauli inayoungwa mkono na wananchi wengi nchini Afrika Kusini ambao wamekuwa wakiandamana kwenye barabara za Afrika Kusini kuhusu huduma mbaya inazotoa serikali lakini mwishoni wanakipigia kura chama cha ANC siku ya kupiga kura.
Wakosoaji wanasema kuwa chama tawala kilinufaika pakubwa sana miaka ya tisini. Lakini sasa kinatishiwa na kukatika kwa mizizi yake na hata kutishia demokasrai nchini humo.

Mauaji ya afisa wa kuchunguza visa vya ufisadi, bila shaka ilikuwa somo kwa Dokta Ramphele kuwa makini katika kauli zake za siku za baadaye.
Hata hivyo kwa kuwa amehusishwa na mtamshi yaliyozua utata kuhusu safari iliyokumbwa na mtafaruku ya Dalai Lama nchini humo, miaka miwili iliyopita inaonyesha kuwa hahofii chochote.
"Haya yote nawafanyia wajukuu wangu, wanangu lakini zaidi sana nawafanyia wananchi wa Afrika Kusini na kuwa lazima ijulikane kuwa wamechoshwa na mambo yalivyo.’’

No comments:

Post a Comment