Tuesday, June 18, 2013

Ujauzito na ulevi nini athari zake?

 

Ujumbe wa kuchanganya kuhusu kiwango cha vileo ambacho mama mjamzito anaweza kunywa wakati akiwa mja mzito, inatatiza wataalamu kuhusu namna ya kukabiliana na utumizi mbaya wa vileo.
Onyo hili limetolewa na wataalamu wanaotaka mambo kuwekwa sawa.
Wataalamu wa afya wanasema kuwa kunywa viwango vya juu vya pombe wakati mama ana ujauzito inaweza kusababisha mimba kutoka , uzani wa chini kwa mtoto, matatizo ya akili na mtoto kuchanganyikiwa anapokuwa.
Lakini wanasema kuwa kukosekana kwa maelezo kuhusu nini maana ya kipimo cha juu au chini cha pombe, ambayo mama anaweza kunywa akiwa na mimba , ina maana wanawake hajaweza kufuata au kutii maagizo au ushauri.
Ilisema kuwa wakunga wanahitaji mafunzo kuweza kuwasaidia akina mama wajawazito kujua vipimo vinavostahili wakati wanapoamua kulewa.


Pombe wakati wa mimba inaweza kuathiri mtoto anavyokuwa baada ya kuzaliwa.
Mfano nchini Uingereza, wanawake wajawazito au wanaojaribu kushika mimba wanashauriwa wanapaswa kujizuia na ulevi.
"nadhani ushauri wa serikali umelegea sana, kwani watu wanaamini kuwa hakuna makosa kwa mwanamke mjamzito kulewa kwa sababu hawajaliharamisha jambo hilo au hajawasema ikiwa ni baya kwa afya ya mama,'' anasema mtaalamu wa ukunga Karen Jewell
Lakini inasema kuwa ikiwa wanawake wataamua kulewa , ni lazima wanywe kwa vipimo vinavyofaa sio zaidi ya glasi mbili mara mbili kwa wiki.

Hata hivyo, mwaka jana , akina mama wajawazito, walionywa na watafiti dhidi ya ulevi kwani itaaathiti akili ya watoto wao.
Katika ripoti iliyofanya nchini Uingereza, ilisema kuwa kuwachanganya watu kuhusu ushauri nasaha kuhusu ulevi kwa wanawake wajawazito sio sawa. Hasa ikizingatiwa kuwa ushari huu hubadilishwa mara kwa mara m,simamo mpya ukitolewa mara kwa mara.
Walisema kuwa ushauri kama huo unawachanga akina mama na kuwafanya kukosa imani na wanaotoa ushauri huo kwa siku za baadaye sio tu kuhusiana na pombe bali pia juu ya maswala mengine ya afya.

Wanawake Uingereza huambiwa kuwa hawapawswi kulewa wakiwa na mimba.
Licha ya viwango vya utumizi mbaya wa vileo kutojulikana , inakisiwa takriban watoto 64,000 nchini Uingereza hupata athari za wazazi kutumia vibaya pombe.
Huduma na msaada kwa wanaotumia vibaya vileo, wakiwa wajawazito, huwa tofauti kabisa na zaidi hulenga matumizi mabaya ya madawa ya kulevya.
Wakati mama mjamzito anapokunywa pombe, viwango vya pombe hiyo huwa juu katika damu ya mwanawe na pia huathiri maini yake.

Ripoti hiyo ilipendekeza kuwa wakunga na wauguzi, waweze kuwapa mafunzo na wao waweze kuwafunza akina mama na kuwashauri kupunguza viwango vya pombe wanayokunywa.
Karen Jewell, mtaamu wa maaswala ya ukunga, walisema kuwa anaamini kuwa serikali zinawatumia ujumbe wa kuachanganya akina mama wajawazito kuhusiana na matumizi ya pombe.
'Nadhani ujumbe wa serikali unapaswa kueleweka kwa sababu akina mama wengi wanachanganywa kwani baadhi wanahisi kuwa hakuna ubaya wowote kwa akina mama wajawazito.' kulewa.
''Lakini baadhi ya wakunga watawashauri akina mama kukoma kulewa kabisa.''

No comments:

Post a Comment