Thursday, June 20, 2013

Simu za Satelite zaharamishwa Borno

 

Simu za Satelite ndizo hutumika sana kwa mawasiliano katika baadhi ya sehemu Nigeria.
 
Jeshi nchini Nigeria limeharamisha umiliki wa simu za mkononi za Satelite katika jimbo moja ambako wanajeshi wanasema wanata kuzuia mawasiliano kati ya wapiganaji wa Boko Haram kufuatia mashambulizi yao ya mapema wiki hii.
Masafa ya Simu za rununu tayari yamebanwa katika jimbo la Borno baada ya sheria ya hali ya hatari kutangazwa katika jimbo hilo mwezi jana.
Msemaji wa jeshi alisema kuwa yeyote atakayepatwa na siku ya mkononi ya Satelite au vifaa vya simu hiyo, atakamatwa.
Wanamgambo wa Boko Haram wamewaua watu 1,600 katika visa kadhaa vya mashambulizi , katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria tangu mwaka 2010.
Rais Goodluck Jonathan, mwezi jana alitangaza sheria ya hali ya hatari katika majimbo matatu yaliyoathirika zaidi kutokana na harakati za Boko Haram, huku maelfu ya wanajeshi wakipelekwa katika jimbo hilo kupambana nao.
Shule mbili zilishambuliwa mwishoni mwa wiki huku takriban wanafunzi 16 na walimu wawili wakiuawa.

Msemaji wa kanali Sagir Musa alisema kuwa wanamgambo wanaofanya mashambmbulizi wanatumia simu za Satelite kupanga mashambulizi yenyewe.
"yeyote atakayepatikana na simu za Suraya, kadi na vifaa vingine atakamatwa,'' alisema kwenye taarifa yake.
Simu za Thuaraya zinatumika sana nchini Nigeria.
Boko Haram, linafanya harakati zake likilenga kushinikiza serikali kuruhusu sheria za kiisilamu kutumia Kaskazini mwa nchiyo ambako kuna iadi kubwa ya waisilmau.

No comments:

Post a Comment