Tuesday, June 4, 2013

Sheria tete ya vyombo vya habari Burundi

 

Waandsihi wa habari wakiitaka serikali kufutilia mbali sheria ya vyombo vya habari.
 
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, ameidhinisha kama sheria mswaada unalenga kudhibiti utenda kazi wa vyombo vyua habari.
Wakosoaji wanasema kuwa Rais anashambulia uhuru wa vyombo vya habari.
Sheria hiyo inaharamisha waandihi wa habari kuripoti kuhusu maswala yanayoweza kuhujumu usalama wa kitaifa, utulivu wa umma na uchumi.
Pia inawalazimisha waandishi wa habari kufichua chanzo cha habari yao pamoja na kuwatoza faini ya zaidi ya dola elfu tano.
Vyombo vya habari pamoja na mashirika ya umma , yamelalamika kuhusu sheria hiyo wakisema kuna utata kuhusu ilivyotungwa na kuwa ni tisho kwa uhuru wa vyombo vya habari.
Sheria hii insemekana kuwa tata na inakuja wakati vyombo vya habari nchini Burundi vinakabiliwa na wakati mgumu.

Hassan Ruvakuki ni mmoja wa waandishi wa habari ambaye amekuwa akizuiliwa kwa muda mrefu huku baadhi ya waandishi wa habari wakilalamika kuhusu kunyanyaswa na polisi. Ruvakuki alikamatwa kwa madai ya ugaidi na kupewa kifungo cha maisha lakini kilipunguzwa hadi miaka mitatu gerezani baada ya kukata rufaa. Ni mwandishi haba ri wa shirika la habari la RFI

No comments:

Post a Comment