Saturday, June 29, 2013

Pesa za misaada zinavyofujwa Afrika

 

Licha ya mamilioni ya dola kutolewa kama msaada wananchi hawafaidiki na miradi ya maendleo
Kamati ya Bunge la Uingereza limepokea taarifa kuwa zaidi ya dola milioni 650 pesa za msaada zilizotolewa na mataifa ya Ulaya kwa bara la Afrika zimetumiwa vibaya.
Kamati ya bunge la malodi kuhusu maswala ya nje, inachunguza ambavyo dola bilioni 1.3 zilizotolewa kama msaada kwa miradi ya maji kusini mwa jangwa la Sahara miaka kumi iliyopita, zilivyotumiwa.
Kamati hiyo iliarifiwa kuwa chini ya nusu ya miradi 23 iliyochunguzwa ilikuwa duni na wala haikutimiza mahitaji ya wananchi.

Matatizo yalitokana na mipango duni na hata wakati wa kuitekeleza miradi mipango haikuwa sawa.
Mkaguzi mmoja wa matumizi ya pesa aliambia kamati hiyo kuwa utafiti wake ulionyesha wazi hali ya miradi mingine ambayo ilifanywa na Muungano wa Ulaya katika mwongo mmoja uliopita.
Miradi ya maji hujumuisha utoaji wa huduma za maji safi, ujenzi wa vyoo hatua ambazo zinazuia kulipuka kwa magonjwa.
Wakaguzi pia waligundua kuwa vifaa vilivyonunuliwa na mameneja wa miradi kama paipu vilikuwa vinahitajika.
Matatizo yanatokana na ikiwa miradi hiyo inaweza kudumu au la.
Katika visa vingine, idadi ya wenyeji wanaopokea mafunzo ni ndogo sana kwa hivyo baada ya miradi kutekelezwa haiwezi kudumu.

Lakini tatizo kubwa zaidi lilikuwa ufadhili au kuwepo mikataba ya kudumu kutoka kwa kamati na serikali za nchi maskini kuhusu namna ya kufadhili mfano hiyo miradi ya maji.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya ustawi Mark Doyle anasema kuwa ikiwa mikataba haiwezi kuwekwa basi itakuwa vigumu kwa matumizi mazuri ya pesa na pia kuna hatari ya pesa za maendeo kuendelea kufujwa.

No comments:

Post a Comment