Tuesday, June 11, 2013

Misri yatoa onyo kali kuhusu Nile

 

Mkutano wa Misri kuhusu mgogoro wa mto Nile.
 
Rais wa Misri Mohammed Morsi amesema kuwa taifa lake litatumia kila mbinu kuhakikisha kuwa Ethiopia inasitisha ujenzi wa bwawa la maji katika mto Nile .
Idadi kubwa ya raia wa Misri millioni 84 imekuwa ikitegemea mto huo kwa maji safi.

Akishangiliwa na wafuasi wake ,Morsi amesema kuwa ijapokuwa Misri haitaki vita haitokubali usalama wake wa maji kuingiliwa kivyovyote.
Tayari kiongozi huyo anapanga kumtuma waziri wake wa maswala ya kigeni nchini Ethiopia ili kuanzisha mazungumzo kuhusiana na swala hilo.
Misri ina wasiwasi kuwa maji ya mto Nile huenda yakapungua kwa kiwango kikubwa iwapo bwawa hilo litajengwa.

Inasema kuwa, kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na mkoloni, ndio taifa linalopaswa kufaidika pakubwa na maji hayo swala linalopingwa na Ethiopia ambayo inasema sheria hiyo imepitwa na wakati.

No comments:

Post a Comment