Tuesday, June 18, 2013

Misri na Ethiopia zaamua kushauriana

 

Ujenzi wa bwawa la Ethiopia katika kingo za mto Blu Nile.
Serikali za Ethiopia na Misri, zimekubaliana kufanya mazungumzo zaidi ili kutuliza mzozo kuhusu ujenzi wa bwawa katika mto wa Blue Nile.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya wizara za mambo ya nchi za nje za nchi hizo mbili.
Waziri wa Ethiopia Tedros Adhanom alisema kuwa nchi hizo mbili zimechagua kusuluhisha mzozo huo kuliko kuendelea kuzozana kuhusu mto huo unazisaidia nchi hizi zote.
Alikutana na mwenzake wa Misri, Kamel Amr baada ya misri kukata mpango wa Ethiopia kujenga bwawa la kuzalishia kawi ya maji.
Misri ina wasiwasi kuwa Bwawa hilo litapunguza viwango vya maji kwa watu wake milioni 84.
Wiki jana rais wa Misri, Mohamed Morsi, alisema kuwa hakutaka vita lakini pia hawezi kuruhusu mtiririko wa maji ya Misri kuhatarishwa kwa ujenzi wa bwawa.
''Hapo awali, matamshi makali yalitolewa kuhusu bwawa hilo wakati pande zote zikiwa na hasira,''alidokeza waziri wa mashauri ya kigeni wa Misri Kamel Amr.
Aidha Klamel aliongeza kuwa ''Tunatafuta njia ya kusuluhisha mzozo kwa sababu ya siku za usoni ili hali iwe nzuri kwetu.''
Hata hivyo rais Morsi alisema kuwa meza ya mazungumzo iko wazi kwa wote watakaoshiriki mazungumzo hayo.
''Tunaanza sarafi ya ushirikiano wa pamoja, '' alinukuliwa akisema bwana Amr.
Kwenye taarifa ya pamoja, bwana Amr na mwenzake wa Ethiopia,Tedros walisema kuwa ushuaino kati ya Misri na Ethiopia,ulisalia kuwa wa undugu na kuwa mazungumzo ya kuangalia hali kuhusiana na bwawa itaendelea.

No comments:

Post a Comment