Monday, June 17, 2013

Mandela aendelea kupata nafuu hospitalini

 

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema hali ya afya ya mzee Nelson Mandela inaendelea kuimarika licha ya kusalia hospitalini katika hali tata.

Bwana Zuma ameyasema hayo wakati sherehe ya sikukuu ya vijana wa Afrika Kusini kwenye jimbo la KwaZulu, ambapo amesema Mzee Mandela anaendelea vizuri na kumudu kuzungumza na familia yake akiwa hospitalini.

Nelson Mandela rais wa zamani wa Afrika Kusini amelazwa akiendelea na matibabu hospitalini mjini Pretoria yapata siku tisa sasa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu ulioathiri mfumo wake wa upumuaji.

No comments:

Post a Comment