Mahakama moja nchini Sweden
imemhukumu kifungo cha maisha jela mtu mmoja kutoka Rwanda kwa kuhusika katika
mauaji ya kimbari yaliyowaacha maelfu ya watu wakiwa wamefariki.
Mahakama hio iliyoko mjini Stockholm ilielezwa kuwa mtu huyo anayefahamika kwa jina Stanislas Mbanenande, ambaye sasa ni raia wa Sweden alishiriki katika mauaji ya watu kadhaa hasa kutoka jamii ya Wa Tutsi kati Mwezi Aprili na Juni mwaka wa 1994.
Mtu huyo pia alipatikana na hatia ya kuongoza kundi la watu wa jamii ya Wahutu wenye msimamo mkali.
Awali majaji kutoka Sweden walisafiri hadi nchini Rwanda ili kupata taarifa kutoka kwa baadhi ya waathiriwa.

No comments:
Post a Comment