Tuesday, June 18, 2013

Madai ya walimu Kenya wanapogoma

 

 
Walimu wa shule za sekondari na taasisi za juu nchini Kenya wameanza rasmi mgomo wao wa kitaifa hii leo baada ya kukosa kuafikia mwafaka na serikali kuhusu kutengewa pesa za kuwalipa marupurupu.
Mgomo huu unakuja baada ya kusomwa kwa bajeti ya serikali wiki jana. Walimu hao wanalalamika kuwa serikali imetenga mabilioni ya pesa kwa ununuzi wa vipakatilishi kwa wanafunzi wa darasa la kwanza badala ya kutumia pesa kwa miradi mingine ambayo ni muhimu zaidi katika sekta ya elimu.
Walimu hao wanasema wataendelea na mgomo wao hadi serikali itakapokubali kuwatimizia matakwa yao.
Pamoja na hilo chama cha walimu hao, kimewataka wanchama wake kusalia nyumbani na kutofunza na badala yake kufika katika makao makuu ya chama cha walimu kwa maagizo zaidi kuhusu hatua wakatazochukua.

Walimu hao wanataka wapewe marupuru ya safari zao pamoja na majukumu ya usimamizi wa shule kuwa sawa na yale wanayolipwa wafanyakazi wengine wa umma.
Pia wanataka swala la kupandishwa vyeo kupewa kipaombele.
Dina gahamanyi alitembelea baadhi ya shule kujionea hali ilivyokuwa.

No comments:

Post a Comment