Thursday, June 13, 2013

Bouteflika afanya mazungumzo na maafisa wake

 

Abdelaziz Bouteflika.
Runinga ya taifa nchini Algeria, imeonyesha picha za kwanza za rais wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika tangu Aprili mwaka huu wakati aliposafirishwa hadi mjini Paris kwa matibabu kufuatia mshtuko wa moyo.
Picha hizo zilimuonyesha bwana Bouteflika, akishauriana na Waziri Mkuu na Mkuu wa Majeshi mjini humo.
Tangu alipopelekwa nchini Ufaransa, kwa matibabu kumekuwa na hali ya wasi wasi kuhusu hali yake.
Katika picha hiyo iliyoonyeshwa siku ya Jumatano, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka sabini na sita alionekana akiwa kwenye mkutano katika makao maalum Kitaifa, iliyojengwa kwa ajili wa raia wakongwe wa taifa hilo ambayo pia inajumuisha hospitali maalum.
Rais Bouteflika alipelekwa katika makao hayo baada ya kutibiwa katika hospitali ya kijeshi ya Val de Grace.

Alionekana kuwa mchovu lakini alikuwa akitabazamu mara kwa mara huku akitumia mkono wake kusisitiza yale aliyokuwa akiyasema.
Shirika hilo la taifa lilisema kuwa rais huyo alifanya mazungumzo na Waziri Mkuu Abdelmalek Sellal na Mkuu wa Majeshi Gaid Sallah kwa masaa mawili na walijadili masuala ya bajeti na masuala mengine ya kiserikali ambayo yanahitaji kuidhinishwa na baraza la mawaziri.

No comments:

Post a Comment