Friday, May 31, 2013

Washukiwa 5 wa mauaji Rwanda wakamatwa

 

Maelfu ya wanyarwanda walipoteza maisha yao katika mauaji ya mwaka 1994.
 
Raia watano wa Rwanda wametiwa nguvuni nchini Uingereza kufuatia ombi la serikali yao kuwataka warejeshwe kujibu mashtaka ya kuhusika na mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu.
Watano hao wamefikishwa mahakamani mjini London hii leo. Baadhi ya waliokamatwa ni mameya watatu wa zamani
Wanatuhumiwa kuongoza mauaji hayo yaliyofanyika nchini Rwanda mwaka wa tisini na nne ambapo mamia ya maelfu ya raia wa kitutsi na baadh ya wahutu waliuawa.
Mnamo mwaka wa elfu mbili na tisa wanne kati ya washukiwa hao walishinda katika rufaa ya kupinga wasirejeshwe nchini Rwanda. Majaji walisema kuwa hawangepewa haki katika kesi hiyo ikifanyiwa nchini Rwanda.

Mmoja wa waliokamatwa ni mwanamume anayetuhumiwa kwa mauaji ya kimbari Vincent Bajinya. Walikamatwa Alhamisi kufuatia ombi la serikali la mshukiwa huyo kurejeshwa nchini Rwnada.
Hakuna habari zaidi kuhusu wahsukiwa wengine wanne waliokamatwa opia kufuatia ombi la serikali ya Rwanda ili waweze kurejeshwa Rwanda kukabiliwa na sheria.
Bajinya anatakiwa kwa kuhusika na mauaji ya Kimbari mwaka 1994. Alikuwa afisa katika kitengo cha maswala ya uzazi wakati mauaji ya kimbari yalipotokea.

Aliwahi kukamatwa kwa mara ya kwanza nchini Uingereza mwaka 2006, lakini alikwepa kurejeshwa Rwanda mwaka 2009 wakati mahakama kuu kuamua kuwa anakabiliwa natisho la usalama wake ikiwa atarejeshwa Rwanda.

No comments:

Post a Comment