Wapenzi wa jinsia moja huhofia kuripoti kwa polisi visa vya dhulma dhidi yao
Muungano wa Ulaya umetoa ripoti
kuonyesha kuwa zaidi ya robo ya wapenzi wa jinsia moja
waliohojiwa
wameshambuliwa ama kutishwa katika miaka mitano iliyopita.
Ripoti hiyo iliandaliwa na wataalamu wa muungano huo kuboresha sera zinazoelekea kutenga watu kutokana na hulka zao za mapenzi.
Watu elfu tisini na tatu wanaoishi
Ulaya walihojiwa kuhusu namna wapenzi wa jinsia moja wanavyochukiwa na
kutengwa. Majibu yao yaliyowasilishwa kwenye mtandao yalionyesha katika
miaka mitano zaidi ya robo walishambuliwa ama kutishwa.
Na shuleni wanafunzi wawili kati ya watatu waliohojiwa walisema kuwa walificha kuwa wao ni wapenzi wa jinsia moja.
Kinachotia wasiwasi ni kuwa zaidi ya nusu yao
hawako radhi kuripoti visa vya kushambuliwa kwa polisi kwa sababu
wanaamini kuwa hakuna kitakachofanyika.
Wanasiasa na watunga sera mia tatu wanakutana
Hague Uholanzi kujadili njia mpya za kuwalinda watu na kuhakikisha kuwa
hawashambuliwi hata wakipendelea mapenzi ya jinsia moja.
No comments:
Post a Comment