Nyumba zilizoharibiwa Baga.
Jeshi la Nigeria halijasema lolote kuhusu madai hayo.
Kuna ripoti za kutatanisha kuhusu idadi ya watu waliouawa huku shirika hilo likidai kuwa watu 37, waliuawa, lakini mashirika mengine yamesema zaidi ya watu mia moja themanini waliuawa.
Wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram, limeendelea mashambulio makali katika eneo hilo, wakitaka kubuniswa kwa jimbo lenye utawala unaozingatia sheria za Kiislamu tangu mwaka wa 2010.
Gari la jeshi lililoshambuliwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria.
Waandishi wa Habari wanasema wanajeshi wa
serikali wameshutumiwa kwa kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa harakati
zao za kuwasaka wapiganaji hao wa waasi.
Shirika hilo la Human Rights Watch limetoa wito kwa utawala wa Nigeria kuchunguza na kuwafungulia mashtaka wanajeshi ambao wanatuhumiwa kuhusika na ghasia hizo za Baga.
Shirika hilo limenadi kuwa uchunguzi wa picha za satelite zimethibitisha kuwa habari zilizotolewa na jeshi kuwa nyumba thelathini ziliharibiwa wakati wa mapigano hayo ya Baga kati ya April kumi na saba na Kumi na nane mwaka huu ni ya uongo.
Wakaazi wa mji wa Baga waliliambia shirika hilo kuwa wanajeshi hao walifanya operesheni kali ya nyumba hadi nyumba baada ya wapiaganaji wa Boko Haram kumuua mwanajeshi ambayo ambaye alikuwa akishika doria katika kituo kimoja cha ukaguzi.
No comments:
Post a Comment