Friday, May 31, 2013

Wabunge wa Kenya wapata pigo

 

Wananchi wa Kenya wakiandamana kupinga wabunge kujiongeza mishahara.

Mahakama nchini Kenya imesimamisha utekelezaji wa nyongeza ya mishahara ambayo wabunge wa nchi hiyo walipendekeza kujiwekea. Chama cha mawakili nchini Kenya kiliwasilisha ombi la kutaka kuwekewa amri ya kisheria wabunge hao siku moja baada ya wabunge hao kupiga kura ya pamoja kutaka wajoingezee mishahara.
Wanaharakati wamekuwa wakipinga jaribio hilo huku wakiandaa maandamano katika barabara za jiji la Nairobi wakimuomba rais asiidhinishe kura hiyo.
Kwa upande wao wabunge hao wameishutumu tume hiyo wakidai kuwa ilivuka mpaka wake kupendekeza wapunguziwe mishahara yao kwa takriban asili mia hamsini kutoka dola elfu kumi kwa mwezi.

Wabunge hao wameelezea hasira zao juu ya tamko la Rais Uhuru Kenyatta na tume ya kudhibiti mishahara ya maafisa wa serikali ambao wanasema waache vitimbi vyao vya kutaka kuongezwa mishahara.
Wanatishia kubadilisha sheria ya idadi ya maafisa wanaoweza kuhudumu katika tume za serikali hadi watatu , kupunguza mishahara ya maafisa wa serikali kwa asilimia hamsini na saba na kuwaondolea wananchi wanaopata chini ya shilingi elfu hamsini kama ajira uwezo wa kutozwa kodi.

Wabunge hao hata hivyo hawaoni ubaya wowote wa kulalamika kuwa mishahara yao inapunguzwa wakisema wanasubiri tume ya bunge kuwalipa mishahara yao ya laki nane na hamsini kutoka laki tano.

No comments:

Post a Comment