Wananchi wamelazimika kutoroka makwao kufuatia mapigano kati ya M23 na wanajeshi.
Awali rais wa benki ya dunia , aliahidi kutoa msaada wa dola bilioni moja kusaidia Congo na nchi majirani zake.
Mkuu wa benki ya dunia, Jim Yong Kim, ambaye pia yuko ziarani DR Congo, alisema kuwa pesa hizo pia zitatumika kwa afya , elimu , biashara na miradi ya kuzalisha umeme.
Takriban watu 20 wameuawa tangu Jumatatu katika makabiliano mapya kati ya serikali na waasi wa M23.
Haya yamekuwa makabiliano ya kwanza kati ya pande zote mbili, tangu waasi wa M23 kuondoka Goma mwaka jana baada ya kuuteka mji huo mwezi Novemba.
Ban anatarajiwa kukutana na wanachama wa kikosi kipya cha umoja wa Mataifa ambacho kimeundwa ili kukabiliana na makundi ya waasi katika eneo la Maziwa Makuu.
Ziara ya bwana Ban inakuja siku moja baada ya benki ya dunia kuahidi msaada wa dola bilioni moja kusaidia kuimarisha maendeleo katika eneo hilo, lakini pesa hizo zitategemea ikiwa pande mbili zinazozozana zitatii mkataba wa amani utakapoafikiwa.
Eneo la Mashariki mwa DRC, limenaswa katika miaka ishirini ya vita kati ya wanajeshi wa makundi ya waasi wanaaminiwa kuungwa mkono na Rwanda pamoja na waliokuwa wahusika wa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.
Kuna matarajio mengi kuwa kikosi hicho cha UN kitaleta utulivu katika eneo hilo lenmye utajiri mkubwa wa madini.
Mapigano yanaendelea kati ya majeshi ya serikali na waasi wa M23 katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Mashambulio yamezidi katika makaazi ya raia.
Wapiganaji hao wa M23 walikuwa wameahidi kusitisha mapigano wakati wa ziara hiyo ya Ban Ki Moon
No comments:
Post a Comment