Mkutano maalumu wa kilele kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (OAU/AU) ulianza Jumamosi asubuhi mjini Addis Ababa.
OAU ilipoanza mwaka wa 1963 ilikuwa na nchi wanachama 33.
Sasa ni jumuiya ya nchi 54.
Nembo ya mkutano ni muibuko wa Afrika na mwenyekiti wa mkutano, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, alisema umoja wa Afrika na chipuko jipya ndio utaamua ajenda ya Afrika katika miaka 50 ijayo.
Sherehe zitaendelea Jumamosi jioni katika ukumbi wa Addis Ababa's Millennium Hall ambapo waziri mkuu wa Ethiopia anaandaa halfa ya usiku huku sherehe zikiendelea kwa muziku na dansi.
Papa Wemba, Salif Keita wa Mali na kikundi cha reggae cha Uingereza, Steel Pulse, wanatarajiwa kutumbuiza wageni.
Tamasha hilo litaonekana kwenye televisheni kubwa zilizosambazwa mjini Addis Ababa.
No comments:
Post a Comment