Hali nchini Syria inaendelea kuzorota huku wahusika kwenye mgogoro wakikosa mwafaka.
Urusi imesema kuwa Syria
imekubali kuhudhuria mkutano wa kimataifa kuhusu hali nchini humo
utakaofanyika mwezi ujao mjini Geneva.
Wizara yake ya mambo ya nje ilisema kuwa
serikali ya Syria, itahudhuria mkutano huo ili watu wa Syria wenyewe
watafute suluhu kwa mzozo unaoendelea nchini humo.
Hatua hii inakuja baada ya juhudi za kutaka pande zote kwenye mgogoro wa Syria kuhusika na mazungumzo ya amani.
Upinzani rasmi nchini Syria, umefanya mazungumzo
kwa siku ya pili, Ijumaa ukitaka kutafuta namna watakavyohusika na
kongamano hilo.
"tunaweza kusema kuwa tumepokea ujumbe kutoka
kwa serikali ya Syria kuwa itahudhuria kongamano hilo kwa niaba ya watu
wa Syria kusukuma ajenda ya amani na mapatano kutumia njia za kisiasa,''
alisema msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi Alexander
Lukashevich.
Marekani imeandaa kongamano hilo ili kutafuta mwafaka wa kisiasa kwa mgogoro wa Syria
No comments:
Post a Comment