Sunday, May 12, 2013

Nawaz Sharif aelekea kushinda Pakistan

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Nawaz Sharif, anasherehekea ushindi na inaelekea atarudi tena kwenye uongozi kwa mara ya tatu.

Nawaz Sharif kwenye kampeni

Baada ya uchaguzi mkuu wa Jumamosi, matokeo yasiyo rasmi yanaonesha kuwa chama chake cha Muslim League kitakuwa na viti vingi kabisa bungeni, lakini kitalazimika kuunda serikali ya mseto.
Bwana Sharif ameahidi kuleta mabadiliko na ameviomba vyama vengine vijiunge naye ili kupambana na changamoto kubwa zinazokabili Pakistan.

Chama cha mcheza kriketi maarufu wa zamani, Imran Khan, kinaelekea kuwa cha pili kwa ukubwa, huku chama tawala cha Pakistan People's Party kinaonesha kimeshindwa vibaya.
Ingawa uchaguzi ulikuwa na ghasia lakini asilimia sitini ya wapigaji kura walijitokeza.
Hii ndio mara ya kwanza katika historia ya Pakistan kwa chama kimoja kilichochaguliwa kukabidhi madaraka kwa chama chengine cha raia.

No comments:

Post a Comment