Friday, May 17, 2013

Mwana Mfalme ashindwa mahakamani Lesotho

 

Wanawake barani Afrika
Maisha ya wanawake nchini Lesotho ni bora zaidi kuliko nchi zote za Kiafrika.
Mahakama ya katiba nchini Lesotho imetupilia mbali kesi ya kutaka watoto wa kike waruhusiwe kuwarithi baba zao kama machifu.
Jaji huyo hata hivyo amesisitiza kuwa katiba ya nchi hiyo haiwabagui wanawake kwani wake za machifu huruhusiwa kuwarithi waume zao.
Wakili wa Afrika Kusini, Priti Patel, anayehusika katika kesi hiyo amesema kuwa uamuzi huo unatanda wingu nyeusi kwa wanawake wa Lesotho.
Lesotho ilikuwa imesifiwa sana kwa namna inavyowapa hadhi ya juu wanawake.
Mnamo mwaka wa 2011, Kongamano la Kiuchumi duniani WEF, liliweka Lesotho katika nafasi ya nane duniani, kwa sera bora za kuwaheshimu wanawake, ikiwa ni juu ya Marekani na Uingereza.
Hii huenda ni kutokana na kuwa Idadi kubwa ya wanawake nchini Lesotho wamesoma na wanafanya kazi nzuri.

Kesi hiyo iliwasilishwa na Senate Masupha, ambaye alinyimwa fursa ya kuwa chifu baada ya babake kufariki na badala yake mamake akamrithi.
"hii inaonyesha kuwa hakuna ubaguzi dhidi ya wanawake lakini ni lazima kwanza wawe katika nafasi fulani kabla hawajarithishwa vyeo.," amesema jaji Ts'eliso Monaphathi, kama alivyonukuliwa na shirika la habari la AFP.

"sidhani kuwa bintiye chifu huyo anaweza kudai kuwa amenyimwa haki zake."
Katika taarifa yake, Bi Patel amesema kuwa ''katiba hiyo imedhihirisha kuwa wanawake wanachukua nafasi ya pili katika jamii nchini Lesotho''.
Ameongeza kuwa uamuzi huo ni unahujumu juhudi zote za awali za kuhakikisha usawa nchini humo.
   

No comments:

Post a Comment