Friday, May 31, 2013

Maandamano Mali dhidi ya Ufaransa

 

Wapiganaji wa Tuareg wanaodhibiti mji wa Kidal.
Maelfu ya watu mjini Gao Kaskazini mwa Mali, wamefanya maandamano wakituhumu Ufaransa kwa kupendelea mahasimu wao wa kabila laTuareg.

Waandamanaji walisema kuwa Ufaransa ina mapendeleo katika kile kinachoonekana kama kabila la Tuareg kuendelea kudhibiti mji wa Kidal
Tuuareg wanaotaka kujitenga wanasema kuwa hawatawaruhsu maafisa wa utawala nchini Mali kuingia Kidal huku uchaguzi ukiandaliwa kufanyika mwezi Julai.
Ufaransa, iliongoza operesheni ya kijeshi kuwafurusha waasi waliokuwa wameteka sehemu ya Kaskazini mwa nchi mapema mwaka huu.

Aidha serikali ya Ufaransa ilianza kuondoa baadhi ya wanajeshi wake 4,000 kutoka nchini humo mwezi Aprili na inapanga kuikabidhi jukumu la ulinzi wanajeshi wa nchi hiyo
Waandalizi wa maandamano yaliyofanyika hapo jana walisema kuwa takriban waandamanaji 3,000 walishiriki kwenye maandamano hayo, ingawa maafisa walisema kuwa idadi yao ilikuwa ndogo.
Maandamano hayo yaliandaliwa na makundi ya kiraia yenye kutoa ulinzii kwa raia walioelezea ghadhabu yao kwa kutohusishwa katika mazungumzo ya kuleta amani Kaskazini mwa nchi.

Makundi hayo, yalisema kuwa kundi la Tuareg, lilialikwa kwenye mazungumzo, ya amani nchini Burkina Faso bila wao kushirikishwa.
"tunataka Ufaransa ituambie wanachonuia," alisema muandamanaji Moussa Boureima Yoro aliyenukuliwa na shirika la habari la AFP
"wanatuchanganya wanaposema kwa upande mmoja kuwa Kidal ni sehemu ya Mali wakati huku kwingine wakijifanya kama sivyo kwa kuepndelea Tuareg.''

Hamil Toure, mmoja wa waandamanaji alimbia BBC kuwa makundi ya vijana yangali yamejihami na kuwa yatazuia uchaguzi kufanyika ikiwa mahitaji yao hayatatimizwa.
Wananchi wengi wa Gao wanalaumu kabila la Tuareg, kwa kuwa chanzo cha mapigano nchini Mali.

No comments:

Post a Comment