Saturday, May 25, 2013

Kocha wa Togo atishia kujiuzulu

 

Wachezaji wa Ivory Coast.
 
Kocha wa Togo Didier Six, ametishia kujiuzulu, ikiwa shirikisho la mchezo wa soka nchini humo halitamlipa dola elfu mia moja na ishirini na nane anazowadai, kutokana na matumizi yake.
Six amesema fedha hizo zinatokana na gharama zake wakati alipokuwa ziarani barani Ulaya kuwachunguza wachezaji.
Kocha huyo sasa ameipa shirikisho la mchezo wa soka nchini Togo, ilaani ya kulipa fedha hizo la sivyo ajiuzulu.
Hata hivyo viongozi wa soka nchini humo wamehoji deni hilo wakisema ni kubwa zaidi.
Msemaji wa shirikisho hilo ameiambia BBC kuwa, licha ya kocha huyo kudai kuwa maafisa wote walifahamu ziara hiyo na dhamira yake, kocha huyo hajawasilisha orodha ya wachezaji aliowatambua wakati wa ziara hiyo.
''Kwa hakika sifahamu tabia ya viongozi wa soka hapa Togo. Mimi sikufanya ziara hiyo kujivinjari'' Alisema kocha huyo ambaye alisaini, mkataba wa kudumu na timu hiyo ya taifa mwaka uliopita.
Hii sio mara ya kwanza kwa kocha huyo kuanzisha malumbano na viongozi wa mchezo huo nchini Togo.

Afisa huyo amehoji baadhi ya matumizi ya kocha huyo katika baadhi ya hoteli za kifahari na tikiti za treni na kusema kuwa hawana wasi wasi wowote kuhusiana na vitisho hivyo, ambavyo kwa sasa anadai wamevizoea.
''Kocha Didier ana mazoea ya kutaka TFA kumrejeshea fedha alizotumia wakati alipokuwa likizoni nchini kwao. Kirasmi alikuwa likizoni na hakuwa na jukumu lingine kwa mujibu wa TFA'' Aliongeza msimaji huyo wa TFA.

Mwaka uliopita, kocha huyo alizozana na TFA kuhusiana na sakata ya kujumuishwa kwa mshambuliaji Emmanuel Adebayor, katika kikosi cha Togo kilichoshiriki katika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika.
Adebayor, alimshutumu kocha huyo, baada ya Togo kubanduliwa nje ya robo fainali ya mashindano hayo nchini Afrika Kusini, akisema kuwa kocha huyo hakuisaidia timu hiyo kwa vyovyote vile.

No comments:

Post a Comment