Monday, May 27, 2013

Kiongozi wa kanisa katoliki Australia azomewa

 

Kadinali Pell anadaiwa kuficha visa vya kudhalalisha watoto kanisani.
 
Kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchini Australia , Kadinali George Pell, ameomba radhi kutokana na tabia ya baadhi ya mapadre kudhalalisha watoto kwa miongo mingi.
Wakati akihojiwa na tume ya bunge inayochunguza visa hivyo , Kadinali Pell amepinga kuchangia katika kuficha vitendo hivyo.

Cardinali huyo alizomewa na watu waliokuwa wamekaa ukumbini wakati akihojiwa huku wakimshtumu kwa kutohurumia waathirika.
Vikao hivyo mjini Victoria vinafanyika kando na tume ya kitaifa inayoskiliza visa vya udhalilishaji wa watoto nchini humo katika mazingira ya kidini au kitaifa.

Kanisa Katoliki, mjini Victoria, limethibitisha kutokea visa zaidi ya mia sita vya kudhalilisha watoto na ambavyo vilifanywa na viongozi wa makanisa , baadhi vikitokea miaka ya 1930.

No comments:

Post a Comment