Imetangazwa kuwa mkuu wa shirika
la usalama la Uingereza, M-I-5, juma lijalo atafika mbele ya uchunguzi
unaofanywa na bunge kujaribu kujua shirika hilo lilikuwa na habari gani
kuhusu vijana wawili waliomchinja mwanajeshi mjini London.
Vijana hao Waislamu wenye msimamo mkali wakijulikana na idara ya usalama lakini M-I-5 itasailiwa zaidi kutokana na madai kwamba ilijaribu kumuajiri mmoja wao, Michael Adebolajo.
BBC iliarifiwa tuhuma hizo na mtu aliyesema kuwa ni rafiki wa Adebolajo.
Alisema watu wa usalama walizungumza na Adebolajo baada ya kijana huyo kurudi kutoka safari nchini Kenya, ambako anadai polisi wa Kenya walimtesa na kumuingilia kwa nguvu kijinsia.
Lakini msemaji wa serikali ya Kenya, Muthui Kariuki, ameshikilia kuwa Adebolajo hakupata kwenda Kenya:
"Sisemi kuwa hakujapata kuwa na magaidi nchini humo.
La, wameingia, sisi tumewakamata tulioweza na wengine pengine walikimbia.
Lakini ninavofahamu mimi kuhusu kisa hichi cha Michael Adebolajo, mimi nasisitiza kuwa huyu hajawahi kuingia nchi hii.
Nakwambia kuwa hatumjui huyu kijana."
No comments:
Post a Comment