Waziri mkuu wa china na mwenzake wa India wameahidi kuunga mkono amani na utulivu.
Zaidi ya miaka hamsini iliyopita tangu nchi hizo zilipigana vita vya muda mfupi, bado nchi hizo hazijakubaliana kuhusu mipaka yao, na India inatuhumu China kwa kudhibiti sehemu kubwa ya ardhi yake.
Waziri mkuu wa India alimpkoea mwenziwe wa China kwa tabasamu na waziri mkuu wa China akisisitiza kwamba lengo kuu la ziara yake ni kujenga imani kati ya nchi zao.
Aidha Li Keqiang amesema kuwa India na China lazima ziimarishe juhudi zake kutuliza mzozo wa muda mrefu katia ya nchi hizo mbili huku akiahidi kuunga mkono juhudi za amani na utulivu
No comments:
Post a Comment