Jeshi la Muungano wa Afrika ambalo limefurusha wapiganaji wa Al Shabaab kutoka Mogadishu,limewadhoofisha wapiganaji hao ingawa hufanya mashambulizi ya mara kwa mara mpakani.
Al-Shabab, linatumia sheria za kiisilamu katika maeneo wanayodhibiti nchini Somalia. Wamefurushwa kutoka maeneo ya mijini ingawa wanaendesha harakati zao katika maeneo ya mashinani.
Mkuu wa polisi, Inspekta David Kimaiyo, aliambia shirika la habari la AP, kuwa watu sita wangali hawajulikani waliko, kufuatia shambulizi la jumamosi usiku.
Sheikh Abdiasis Abu Musab,ambaye ni msemaji wa shughuli za kijeshi za al-Shabab, aliambia shirika la habari la Reuters kuwa siku ya Jumamosi waliweza kuingia kilomita 35 ndani ya Kenya na kuvamia kambi za polisi.
Mtandao mmoja wa kundi hilo ulikuwa na ahabri kuwa watu wawili walitekwa nyara na kuingizwa Somalia.
Mkuu wa wilaya karibu na kambi ya Dadaab, Albert Kimathi, alithibitisha mashambulizi hao mawili dhidi ya vituo vya polisi.
Wanamgambo hao wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mpakani nchini Kenya tangu mwaka 2011 ambapo majeshi ya Kenya kwa ushirikiano na wanajeshi wa AU , walipoingia Somalia kupambana na wanamgambo wa Al Shabaab
No comments:
Post a Comment