Watu wengi zaidi wamejiandikisha
kushiriki kwenye marathon ya Madrid, Uspania, ya Jumapili ya mwisho wa
Aprili baada ya shambulio la bomu kwenye marathon ya Boston siku ya
Jumatatu.
Waandalizi wa mbio hizo wanasema watu waliojiandikisha ilizidi mara nne baada ya shambulio la Boston.
Mkuu wa kamati ya Olimpiki ya Uspania ambayo inajitayarisha kuomba kuandaa Olimpiki ya mwaka wa 2020, alisema wanaoshiriki kwenye marathon wakiongezeka ndio sifa kubwa ambayo watu wa Madrid wanaweza kuupa mji wa Boston.
No comments:
Post a Comment